Majila ya jioni chapu nikarudi Nyumbani uku nikiwa na shauku sana na kula chakula kilichopikwa na Tamika, Sijui Kwanini Nilimwambia afanye kitu Kama iko ikiwa tayali Nyumbani Tuna mfanya kazi kwaajili ya kutupikia na majukumu mengine mengine.
Nilifika Nyumbanina kwenda kuoga mwisho nikarudi zangu sebuleni na Tamika hakuwa mbali akaja na kunitengea chakula utazani anamtengea mume wake wa Ndoa vile.
“Asante sana Tamika”
Nilizungumza baada ya Tamika kumaliza kuniwekea chakula.
“Ungana na Mimi “
Nilimwambia Tamika baada ya kumuona Kuwa anataka kwenda chumbani kwake, kWa utulivu Tamika akajibu.
“Aaaah niko Sawa aiseeeh nimetoka kula musa sio mrefu boss wangu “
“Mmmmh Tamika jamani, huo uongo umeanza lini jamani, jumuika na Mimi jamani “
“Niko Sawa boss “
“Hapo kwenye boss sasa, Naomba nite Ezra Bwana “
“Sawa”
****
Siku ziliendelea kwenda uku Mimi na Tamika tukiwa watu wa Karibu sana Tena sana, Yaani Tamika sikuwa na kila aina ya vibe , kila siku zilivyozidi kwenda ndio nilizudi kuona uzuri wa Tamika ambao amekuwa akiufucha kWa mavazi yake mabaya, lakini pia na kujiweka Kama mwanaume ambaye umri umeenda.
Yaani kumkuta Tamika akiwa sana nywele zake Ndefu ni kazi sana, Mara nyingi Tamika amekuwa ni mtu wa kufunika nywele zake kwenye mzula ambao ilipauka sana.
Siku moja ikiwa ni siku ya weekend, nilitoka zangu mjini na kuchukua vizawadi kwaajili ya Tamika, lakini pia nilimchukualia nguo nzuri sana kwani nilitaka Kwenda nae club kwa siku hiyo.
Majila ya usiku Kama kawaida nikatoka nikiwa na Tamika, Walahi alipendeza sana, mavazi ambayo nilimjumulia yalikuwa on top Yaani, ukiwa kuangalia na shape yake ndio kabisa Yaani niliweza halafu nikaweza tena.
“Kwahiyo Tamika wewe utumii Pombe kabisa ?”
Nilimuuliza Tamika tukiwa kwenye gari.
“Ahşaba Ezra Bwana nimeamka uamini hivi si ndio ? Yaani Mimi na Pombe ni Kama radhi na mbingu atuwezi kushikana kabisa, lakini ikitokea siku nimekunywa nakuomba Kama ni Nina Siri zako Walahi nazizagaza 😂🙌”
“We mjinga kweli Mbona kuzizagaza jamani 😁”
Hizo zilikuwa ni story za hapa na hapa kati yangu na Tamika, yooooh huyu girl ananıza vibe la maana kabisa na kuna muda ni Kama nilianza kumkwepa Demi wangu hivi kwaajili ya kutumia muda mzuri na Tamika.
Hatimaye tulifika club na kulikuwa Bna vibe Kama lote, kila mtu alikuwa bize na vinywaji lakini pia na kunywa na kula, Tamika alionekana Kuwa sio mtu wa starehe ata kidogo, Mara nyingi alikuwa chini akiangalia mambo yanayoenda.
Muda huo huo akaingia mkaka Fulani hivi, huyu kaka jamani yuko hot, muonekano wake ni kila mwanamke Anadata nae, na Kama yuko vizuri sana kila demi anapita Nae na yote hii ni kwakuwa alikuwa nampesa na hapo club alijulikana Kama PEDESHEE.
Siku hiyo pedeshee aliingia akiwa na pisi moja Kali sana, muda huo huo Tamika akanyanyuka kwenye kiti chake na kumsogelea PEDESHEE na kumchezeshea kibao kimoja Matata sana.
Kiukweli nilishtuka sanana haraka nikamuwai na kumuuliza.
“Kuna nini ?”
“Ezra Kaa mbali Tena mbali sana”
Alizungumza Tamika Ka hasira sana kisha akamgeukia pedeshee na kumchezeshea kichwa cha mwana ukome, kila mtu alishangaa ikiwemo mimi.
Kabala sijaingilia kati kwaajili ya kutuliza vulugu Tamika akamuuliza PEDESHEE.
“Hapa ndio marekaji Issah ?”
Kwanza macho yalinitoka Walahi, tangu NAKUJA huyu Issah hakuwai ata kutoka nje ya Mikoa halafu Leo hii anaulizwa hapa ndio Marekani.
KWa sauti ya kejeli PEDESHEE akajibu.
“Mshangazi Kaa mbali na Mimi Sawa huu ni muda wa mabinti “
Weeeeh kitendo cha yeye kumuita Tamika mshangazi kilinikasilisha na nikajikuta Nikiununua ugomvi, woiiiiih Sijui nilipatwa na nini lakini sio kWa hizi ngumi ambazo nilianza kumchezeshea huyu pedeshee.
Tamika akaniwai na kunitoa nje, lakini Tamika hakuwa Sawa kabisa, kitendo cha kutoka nje tu Tamika aakajitupia chini na kuanza kulia, nyie nilimuonea huruma sana Tamika.